Proverbs 23


1Uketipo kula chakula na mtawala,
angalia vyema kile kilicho mbele yako,

2 na utie kisu kooni mwako
kama ukiwa mlafi.

3 aUsitamani vyakula vyake vitamu
kwa kuwa chakula hicho ni cha hila.


4 bUsijitaabishe ili kuupata utajiri,
uwe na hekima kuonyesha kujizuia.

5 cKufumba na kufumbua utajiri hutoweka,
huwa kama umepata mabawa ghafula,
ukaruka na kutoweka angani kama tai.


6 dUsile chakula cha mtu mchoyo,
usitamani vyakula vyake vitamu,

7 ekwa maana yeye ni aina ya mtu
ambaye kila mara anafikiri juu ya gharama.
Anakuambia, “Kula na kunywa,”
lakini moyo wake hauko pamoja nawe.

8 Utatapika kile kidogo ulichokula,
nawe utakuwa umepoteza bure
maneno yako ya kumsifu.


9 fUsizungumze na mpumbavu,
kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako.


10 gUsisogeze jiwe la mpaka wa zamani
wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima,

11 hkwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu,
atalichukua shauri lao dhidi yako.


12 iElekeza moyo wako kwenye mafundisho
na masikio yako kwenye maneno ya maarifa.


13 jUsimnyime mtoto adhabu,
ukimwadhibu kwa fimbo, hatakufa.

14 kMwadhibu kwa fimbo
na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini
Mautini maana yake ni Kuzimu.


15 mMwanangu, kama moyo wako una hekima,
basi moyo wangu utafurahi,

16 nutu wangu wa ndani utafurahi,
wakati midomo yako
itakapozungumza lililo sawa.


17 oUsiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi,
bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Bwana.

18 pHakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako,
nalo taraja lako halitakatiliwa mbali.


19 qSikiliza, mwanangu na uwe na hekima,
weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa.

20 rUsiwe miongoni mwa wanywao mvinyo,
au wale walao nyama kwa pupa,

21 skwa maana walevi na walafi huwa maskini,
nako kusinzia huwavika matambara.


22 tMsikilize baba yako, aliyekuzaa,
wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee.

23 uNunua kweli wala usiiuze,
pata hekima, adabu na ufahamu.

24 vBaba wa mwenye haki ana furaha kubwa,
naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia.

25 wBaba yako na mama yako na wafurahi,
mama aliyekuzaa na ashangilie!


26 xMwanangu, nipe moyo wako,
macho yako na yafuate njia zangu,

27 ykwa maana kahaba ni shimo refu
na mwanamke mpotovu ni kisima chembamba.

28 zKama mnyang’anyi, hungojea akivizia,
naye huzidisha wasio waaminifu miongoni mwa wanaume.


29 aaNi nani mwenye ole?
Ni nani mwenye huzuni?
Ni nani mwenye ugomvi?
Ni nani mwenye malalamiko?
Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu?
Ni nani mwenye macho mekundu?

30 abNi hao wakaao sana kwenye mvinyo,
hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.

31 Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu,
wakati unapometameta kwenye bilauri,
wakati ushukapo taratibu!

32 Mwishowe huuma kama nyoka
na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.

33 Macho yako yataona mambo mageni
na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka.

34 Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari,
alalaye juu ya kamba ya merikebu.

35 acUtasema, “Wamenipiga lakini sikuumia!
Wamenichapa, lakini sisikii!
Nitaamka lini
ili nikanywe tena?”
Copyright information for SwhKC